Epuka Chaguomsingi

ili kuboresha ustawi wako wa kidijitali

Pakua na chapisha mwongozo huu. Shiriki uzoefu wako wa kuchuja taarifa/maudhui, wasiliana, au pata msukumo wa shughuli kwa kumwandikia Safa kupitia datadetox@tacticaltech.org!

Ni lini mara yako ya mwisho ambayo ulikaa siku nzima “pasipo” kutumia intaneti?

Uwapo mtandaoni, haupo peke yako. Kwa wastani mtu mmoja hutumia simu zaidi ya mara 2,600 kila siku (chanzo). Ufanyapo kitu mara kwa mara unge tamani kuona thamani ya unachofanya. Lakini wawezaje kutambua kuwa muda unaotumia kwenye kifaa chako ni muda sahihi?

Yapasa kutambua kuwa ugumu wa kukaa mbali na teknolojia sio kosa lako! Amini usiamini, programu na tovuti zako pendwa zimetengenezwa ili zikuvutie kimuonekano, kwa rangi na sauti na kukufanya uendelee kutumia tena na tena.

Pia programu na tovuti zimetengenezwa kuwaelekeza watumiaji kupata kile wanachofikiria wanakihitaji. Vitufe husisitiza uhakikishaji na jumbe huandikwa kumvutia mtumiaji. Vivyo hivyo, vyombo vya habari hutumia vichwa vya habari vyenye mvuto ili kuteka hisia za watumiaji.

Je, unataka kufahamu jinsi ya kuwa na uwiano kati ya maisha yako ya mtandaoni na nje ya mtandao? Kipengele kifuatacho kitakufundisha jinsi ya kusafisha taarifa zako mtandaoni.

Hapa, utajifunza jinsi ya kukwepa changamoto za kimtandao na kutumia teknolojia kukuinua badala ya kukudidimiza. Hakuna “jibu sahihi” la jinsi gani (au mara ngapi) unapaswa kutumia vifaa vyako vya kidijitali. Chagua unachofikiri ni sawa.

Sasa tuanze!


1. Makinika

Hiki kidokezo ni kigumu kuliko unavyodhani. Umakini huhitaji mazoezi ya kila siku. Ni kama vile misuli ya ubongo wako inavyohitaji kuzoeshwa kufanya kazi ili kujenga uwezo. Unaweza kuanza kwa kutathmini uhusiano wako na teknolojia unayotumia

Unatumia muda gani kwenye simu yako?

Kama hujaridhika na jibu lako, basi kuna mipangilio na mikakati unayopaswa kufuata ili uweze kudhibiti matumizi yako ya teknolojia.

Kama lengo lako ni kutumia muda mchache kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram, au Snapchat, basi badili mipangilio na ruhusa za matumizi ya programu hizo ili kuzifanya ziendane na mahitaji yako. Programu zingine kama vile Instagram zina hadi chaguzi zinazokukumbusha kuwa umefikia kikomo cha muda wa matumizi ya programu hiyo kwa siku husika.

Instagram:

  • Wasifu →
  • logo Menyu →
  • Mipangilio
  • Akaunti
  • Shughuli yako
  • Weka Ukumbusho wa kila Siku

Kama ukigundua milio, mitetemo ya simu yako au kupigiwa simu, kunaingilia maisha yako ya kawaida, waweza kuiweka simu yako kwenye hali ya ukimya, na kisha kuifunika, kuiweka mfukoni, ndani ya begi au pochi ili iwe mbali na upeo wa macho yako.

Pia kuna aplikesheni zinazoweza kukusaidia kupima matumizi yako ya simu. Vifaa vya Android na iPhone vina huduma za kutoa taarifa ya tabia za matumizi ya simu yako kupitia Ustawi wako wa Kidijitali kupitia Google na kusasisha mfumo wa iOS. Huduma hizi zitakuonesha ni mara ngapi umetumia simu yako, na kukuelekeza namna ya kudhibiti matumizi ya simu yako.

Kupata dondoo zaidi, pitia mwongozo wa Makinika (Hata katika matumizi yako ya simu).


2. Tambua mbinu za ubunifu mitandaoni

Ubunifu unaoshawishi watumiaji wa mitandao, unaojulikana pia kama “mifumo ya udanganyifu”, hugusa saikolojia ya mwanadamu ambayo hutumika kukushawishi kufungua akaunti, kununua kitu, au kutoa taarifa zako binafsi mitandaoni, tofauti na vile ulivyofikiria au kutarajia.

Mara nyingi mbinu hizi za ushawishi wa kibunifu hutumia rangi husika, mipangilio ya vitufe, maneno yasiyoonekana vizuri, au taarifa za mkato. Mara nyingi hizi mbinu huonekana kirahisi, lakini wakati mwingine ni ngumu kuzigundua. Waweza kuwa umewahi kuzigundua unapojiandikisha kupata huduma mitandaoni au kufanya manunuzi mitandaoni.

Sababu za uwepo wa mbinu hizi za ubunifu kila mitandaoni ni ushahidi kwamba zinafanya kazi – zinatushawishi kubonyeza, kujiandikisha kupata huduma na manunuzi mitandaoni, na kurudia tena na tena. Kadri unavyozidi kufahamu mawaidha na upotoshaji wa hila uliopachikwa katika tovuti unazotumia, ndivyo utakavyozidi kuwa mjuzi na mwenye taarifa.

Kuna baadhi ya vitu waweza kufanya kuzizidi ujanja programu zako.

Tambua unaposhawishiwa: Kwanza kabisa, inabidi ufahamu hizi mbinu za ushawishi. Soma kuhusu baadhi ya hizi mbinu hapa, na fuatiliaTwitter feed au hashtag kupata taarifa mpya kuhusu hizi mbinu za ushawishi.

Piga picha skrini na kusambaza: Unapokutana na kurasa zenye miundo ya kiushawishi mitandaoni, zipige picha na kuwasambazia marafiki zako (tafadhali zingatia kuficha taarifa za utambulisho wako binafsi kabla ya kusambaza – ulinzi wa faragha yako ni muhimu!). Waweza pia kuziomba kampuni za kurasa husika mitandaoni kubadili mbinu zao.

Piga picha skrini na kusambaza: Unapokutana na kurasa zenye miundo ya kiushawishi mitandaoni, zipige picha na kuwasambazia marafiki zako (tafadhali zingatia kuficha taarifa za utambulisho wako binafsi kabla ya kusambaza – ulinzi wa faragha yako ni muhimu!). Waweza pia kuziomba kampuni za kurasa husika mitandaoni kubadili mbinu zao.

Kuona mifano ya mifumo ya kidanganyifu, na kujifunza zaidi jinsi ya kuitambua mifumo hiyo, soma makala ya Intaneti Ilinifanya Nifanye Hivyo: Elewa Kuhusu Miundo Yenye Utata.


3. Endelea kuwa mwenye kufuatilia habari

Kama ambavyo unaweza kujifunza kuwa mjanja zaidi ya teknolojia na miundo iliyoundwa kukufanya uendelee kutumia simu, vivyo hivyo unaweza kujifunza jinsi ya kugundua taarifa za uongo au za kupotosha.

Hadi hivi sasa, utakuwa unafahamu kuhusu changamoto za ‘taarifa za upotoshaji’ na ‘taarifa za uongo’. Unaweza kujifunza kuhusu taarifa za upotoshaji ukiwa na tabia ya kujiuliza maswali kwa kina kuhusu kila habari unayoisoma, hasa kama ni taarifa ya kushangaza, kukera au yenye utata.

Mwisho wa siku, unapaswa kuhakiki usahihi wa kila taarifa – hasa kama una mpango wa kusambaza taarifa husika kwa familia au marafiki.

  • Taarifa hii imetoka kwenye tovuti gani?
  • Nani mwandishi wa hii taarifa (na aliiandika lini)?
  • Je, makala nzima inahusu nini, ukiachana na kichwa cha habari?
  • Mwandishi ametumia vyanzo gani?

Kama unadhani ni taarifa ya upotoshaji na unataka kuzuia isisambae, mitandao mingi ina huduma ya kuripoti taarifa za upotoshaji. Unaweza pia kuamua kuendelea kufuatilia ukurasa huo uliochapisha hiyo taarifa au la.

Kujifunza zaidi kuhusu taarifa za upotoshaji, soma kuhusu Washa Taa: Fahamu Ukweli Kuhusu Intaneti.


4. Fanya Sauti Yako Isikike

Kama haufura hishwi na ushawishi au taarifa za upotoshaji kwenya tovuti unazopitia mara kwa mara au programu unazotumia, waweza kutuma barua pepe, kuandika twiti, na kuyajulisha makampuni ya mitandao husika kuwa hukubaliani na mbinu zao. Makampuni yanaposisitizwa kuchukua maamuzi sahihi kutoka wateja wao, kuna uwezekano wa wao kubadilika.

Kama haufura hishwi na ushawishi au taarifa za upotoshaji kwenya tovuti unazopitia mara kwa mara au programu unazotumia, waweza kutuma barua pepe, kuandika twiti, na kuyajulisha makampuni ya mitandao husika kuwa hukubaliani na mbinu zao. Makampuni yanaposisitizwa kuchukua maamuzi sahihi kutoka wateja wao, kuna uwezekano wa wao kubadilika.

Kwa vidokezo zaidi kuhusu namna ya kugundua mbinu za ubunifu wa mitandao, soma makala ya Intaneti Ilinifanya Nifanye Hivyo: Elewa Kuhusu Miundo Yenye Utata.


5. Eneza Neno

Ipitishe! Hiki ni kidokezo rahisi kusahau, lakini kinaweza kuwa na athari kubwa. Waambie marafiki, familia, na wafanyakazi wenzako kuhusu mambo hayo unayoona, na hata uwaombe wajiunge nawe katika zana ya kuondoa sumu mtandaoni!

Kila mtu anapambana na kudhibiti tabia zao za simu. Kilicho muhimu ni kupata njia ambayo inahisi sawa kwako na inafaa mtindo wako wa maisha. Jaribu hadi upate inayokufaa, kisha usasishe mazoea yako kadri mahitaji yako yanavyobadilika kadiri muda unavyopita. Hakuna saizi moja-inafaa-yote suluhisho.

Na hatimaye, wasiliana na chaguo zako za teknolojia na wale walio karibu nawe. Tuseme hutapatikana kwenye programu yako ya messenger kila siku baada ya 8 Mchana kwa sababu hapo ndipo utakapoanzisha utaratibu wako wa bila skrini: waambie familia yako na marafiki ili waweze kukupigia simu badala yake.

Weka mazungumzo wazi, uliza maswali, na unaweza kuishi maisha yenye usawa mtandaoni ambayo yanakufaa.

Ikiwa hatua hizi zilikufaa na unahisi kuwa na usawaziko zaidi, basi kwa nini usijaribu Simu mahiri kwa Mazoea Mahiri?

Ilisasishwa mara ya mwisho mnamo: 10/11/2022